Uga wa Kamkunji, ambapo mechi za mitaa za eneo la Nakuru mashariki zinaandaliwa sasa watajwa kuwa kero kwa wachezaji na mashabiki wanaohudhuria mechi hizo.
Kulingana na mashabiki, uga huo uko katika hali mbaya kwani hujaa maji na matope baada ya mvua kunyesha, hivyo basi kutatiza mechi zinazosakatwa kwenye uga huo.
Uwanja huo, ambao aslimia tisini yake hauna nyasi umekua ukiandaa mechi za mitaa zaidi yamiaka mitano sasa.
Harrison Amanda, shabiki sugu wa timu ya Bondeni aliwaomba wasimamizi wa mechi hizo kuhamisha mechi hadi uwanja wa Kisulisuli, akitaja uwanja huo kama ulio katika hali nzuri ya kuandaa mechi hizo.
"Uwanja wa Kisulisuli uko katika hali nzuri sana na naomba waandalizi wamechi hizi kuziamisha ili sisi kama mashabiki tuweze kufurahia mchezo huu," alisema Amanda.
Wachezaji pia wamelaumu uwanja huo kwa matokeo mabaya kwa timu zao huku wakiomba waandalizi wa mechi hizo kurekebisha uwanja huo kwa kuchimba mitaro kando kando ili kuzuia maji kusimama kwenye uwanja huo.
Timu kadhaa zimelaumu uwanja huo kwa matokeo mabaya yao.