Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Daktari wa kitengo cha maradhi ya kisukari amesema kuwa uhamasishaji zaidi wapaswa kufanywa, licha ya kubainika kuwa idadi ndogo ya watu ndio hawajafahamu kuhusu ugonjwa huo unaokua kwa kasi ulimwenguni.

Wito huo umetolewa huku ulimwengu ukitarajiwa kuadhimisha siku ya ugonjwa wa kisukari siku ya Jumamosi.

Akizungumza siku ya Ijumaa, daktari wa kitengo cha maradhi ya kisukari katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Pwani Dkt Cyprian Muyodi alisema kuwa idadi kubwa ya watu wanajua dadili za maradhi hayo ilikinganishwa na miaka ya nyuma.

Aidha, alisema kuwa wagonjwa wengi hujitokeza kila uchao kutafuta matibabu ya ugonjwa huo ambao unahangaisha wengi.

Vilevile alieleza kuwa uhamasishaji wa mara kwa mara kuhusu maradhi hayo umesaidi pakubwa katika kuwajulisha wakazi kuhusu ugonjwa huo.

“Uhamasishaji zaidi kuhusu ugonjwa wa kisukari wapaswa kuendelea kufanywa ili wakazi wajue jinsi ya kujikinga sawia na kupunguza kuenea kwa maradhi hayo,” alisema Dkt Muyodi.

Wakati huo huo ametoa wito kwa kila mtu kujitokeza ili kujua hali yake ya kiafaya ili kuepuka maradhi mbalimbali.