Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Katibu wa Wizara ya Uchukuzi John Musonik amewahakikisha wakaazi wa Pwani kuwa mpango wa kujengwa kwa barabara ya Dongo Kundu ungali upo.

Hana yanajiri baada ya wakaazi, hasa kutoka eneo la South Coast, kulalamikia changamoto za usafiri, kufuatia kulazimika kutegemea feri kuvushwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Akiongea na waadhishi wa habari siku ya Jumatano kwenye ofisi kuu za Halmashauri ya Bandari nchini KPA, kwenye kikao na maafisa kutoka nchi ya Uhabeshi, Mosonik alisema kuwa mpango wa kutengeza barabara hiyo uko hai na ni muda mfupi tu kabla ya mradi huo kuanzishwa rasmi.

Alisema kuwa mradi huo utawafaa wakazi pamoja na wenye magari katika eneo zima la South Coast, ambao wamekuwa wakihangaika kwa muda mrefu kwa kutegemea mfumo mmoja wa kuwaunganisha baina ya maeneo ya kisiwani.

Musonik aidha ameweka wazi kuwa serikali itahakikisha kuwa miradi ya kukarabati barabara na kutengeza nyingine mpya za kuingia na kutoka katika eneo la bandari kama vile ile ya Portreiz inatekelezwa.

Ukarabati wa miundomsingi katika bandari kuu ya Mombasa unalenga kurahisisha usafiri wa malori ambayo yanaingia na kutoka bandarini.

Hatua hiyo inanuia kuzuia msongamano wa magari yanayoingiza na kutoa shehena bandarini.