Serikali imerejelea kauli yake ya kujenga barabara ya Dongo Kundu ili kupunguza shughuli nyingi katika kivuko cha feri cha Likoni.
Serikali imetenga shilingi milioni saba kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Dongokundu ili kupunguza msongamano wa magari na watu kwenye kivukio hicho.
Akizungumza siku ya Jumamosi kwenye hafla ya mchango kwa ajili ya ujenzi wa maktaba ya shule ya Liwatoni mjini Mombasa, kiongozi wa walio wengi katika bunge la kitaifa Aden Duale alisema tayari bunge limeshapitisha kutolewa kwa fedha hizo kufuatia malalamishi ya wakazi wanaotumia kivuko hicho.
Duale ailongeza kuwa barabara hiyo itarahisisha na kuimarisha usafiri na kuimarisha biashara jijini Mombasa na kaunti nyinginezo pamoja na mataifa jirani.
Duale alisema ujenzi huo huo utaanza mara moja.