Ukosefu wa vyoo katika makaburi ya Nakuru Kusini ni kero kwa wakaazi wanaoishi karibu.
Katika mahojiano, wakaazi hao wakiongozwa na Irene Nyasembo wanasema kuwa swala hilo limekuwa kero wakati wa mazishi.
"Wanaokuja mazishi kwa makaburi haya wametukera sana, kila mara unakutana na mtu eti anatafuta choo," Nyasembo alisema.
Ni kutokana na hilo ambapo walitoa wito kwa serikali ya kaunti ya Nakuru kuingilia kati swala hilo na kuhakikisha kwamba kuna vyoo vya kutosha katika makaburi haya ya Manyani.
Tangu kufungwa makaburi ya Nakuru kaskazini, shughuli zote za mazishi hufanyika makaburi ya Nakuru kusini.