Share news tips with us here at Hivisasa

Baadhi ya viongozi wa eneo la Pwani wanaukashifu vikali uongozi wa wa muungano wa Jubilee, huku wakiutaja muungano huo kutojali na kutimiza mahitaji ya wakaazi wa Pwani.

Wakiongozwa na mwakilishi wa wadi ya Sabaki kaunti ndogo ya Magarini Edward Dele, viongozi hao wamekashifu mienendo  na matamshi ya yasiyo na uzalendo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa muungano huo kwa misingi kwamba muungano huo utafanya kila uwezalo kuchukua uongozi wa mwaka 2017.

Dele ameongeza kuwa viongozi wa Pwani hawatakubali uongozi huo mbaya, na kuahidi kuwa kutetea maslahi ya wananchi yakiwemo masuala ya ardhi na ajira miongoni mwa masuala mengine.

Kauli hii inajiri siku chache baada ya mmoja wa viongozi wa muungano wa Jubilee, Suleimana Shabali kutamka kwamba muungano huo wa Jubilee utatumia njia yoyote ikiwemo kuiba ama kununua kura kuhakikisha muungano huo unabaki kuwa madarakani mwaka wa 2017.

Muungano wa upinzani umekosoa serikali ya Jubilee kwa kukithiri kwa visa vya unyakuzi wa ardhi na ufisadi wa aina mbali mbali ikiwemo sakata ya Eurobond na kupotea kwa pesa za shirika la huduma kwa vijana, NYS miongoni mwa maovu mengine.