Makampuni ya mbao na wezi wa miti wametajwa kama kizingiti katika shuguli ya kuhifadhi misitu katika kaunti ya Nakuru.

Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Afisa mkuu katika wizara ya mazingira ya kaunti ya Nakuru, Nelson Tanui amesema kuwa makampuni ya kutengeza mbao na wezi wa miti wamechangia pakubwa katika kupungua kwa kiwango cha miti katika misitu ya serikali.

Akiongea Jumanne jioni aliopongoza shuguli ya upanzi wa miti katika eneo la kabatini eneo bunge la Bahati,Tanui alisema kuwa makampuni hayo huwatumia wezi wa miti kuingia misituni na kukata miti kiharamu.

“Hawa watu wa makampuni ya mbao wanatutatiza wa sababu ni hao wanao nunua miti kutoka kwa hwa wezi wanaoiba miti yetu. Na hata hayo makampuni yanakata miti kwa wingi sana kuliko vile wanavyopanda na hii inatatiza juhudi zetu za kuhifadhi misitu ya serikali,” alisema Tanui.

Aliyataka makampuni ya mbao kushirikiana na serikali ya kaunti katika kupanda miche zaidi katika misitu ili kuhifadhi mazingira na kulinda kizazi cha kesho.

“Kama haya makampuni yangeshirikiana na serikali basi tungekuwa mbali sana katika upanzi wa miti na tunawataka wachangie katika kuhifadhi mazingira kwa kukataa kununua miti kutoka kwa wezi na pia kupanda miche mingi mara wanapokata miti ya kutengeneza mbao,” alisema.

Wakati wa shuguli hiyo zaidi ya miche 500 ilipandwa katika eneo hilo katika harakati inayoendelezwa na serikali ya kaunti ya Nakuru kuimarisha kiwango cha misitu katika kaunti ya Nakuru.