Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Idadi ya visa vya uhalifu katika kaunti ya Kisumu imepungua kwa asilimia kubwa kutokea mwezi Septemba hadi mwezi Januari mwaka huu.

Haya ni kwa mujibu wa Gavana wa Kaunti ya Kisumu Jacktone Ranguma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kwanza cha bunge la kaunti ya Kisumu baada ya kukamilika kwa mapumziko ya mwezi Desemba, Ranguma alisema kuna ushirikiano kati ya idara ya usalama, serikali kuu na kubuniwa kwa kitengo cha polisi wa kushugulikia maswala kwa dharura.

''Serikali yangu itaendelea kutilia mkazo usalama wa wakazi wa kaunti ya Kisumu, na kwa ushirikiano na serikali kuu tutafanikiwa katika juhudi hizo,'' alisema Ranguma.

Kando na usalama, Ranguma alieahidi kuwa serikali yake itajizatiti kuimarisha sekta ya afya, huku maeneo yatakayoangaziwa zaidi yakiwa Kombewa, Papo Nditi, Chula Imbo, Migosi, Kombewa miongoni mwa maeneo mengine.

''Kinachotakiwa ni kila mmoja ikiwemo serikali ya kitaifa na ya kaunti kutokuwa na mwingiliano katika majukumu ya kila mmoja, majukumu ya serikali za kaunti ikiwemo ukarabati wa barabara haufai kuvutwa upande wa serikali kuu na kudaiwa kuwa baadhi ya barabara zilizokarabatiwa na kaunti zimesimamiwa na CDF," alisema Ranguma.

Kadhalika, kiongozi huyo aliahidi kuangazia changamoto za wafanyibiashara katika soko za Kisumu hasaa maeneo ya Kisumu ya kati na maeneo Milimani.