Share news tips with us here at Hivisasa

Kikao cha kutafuta mwafaka wa mgomo na maandamano ya wanafunzi wa chuo cha anuwahi cha Mombasa sasa kimehahirishwa kwa muda usiojulikana.

Hii ni baada ya wasimamizi wa chuo cha TUM kukosa kuhudhiria kikao hicho siku ya Jumatatu katika bunge la kaunti ya Mombasa.

Rais wa muungano wa wanafunzi wa chuo hicho Desmond Ocharo alionyesha kusikitishwa na hatua ya usimamizi wa chuo hicho kwa kukosa kufika kwenye kikao hicho, na kuongeza kuwa usimamizi huo unajikokota kutafuta suluhu la kudumu katika chuo hicho.

Wakati huo huo, naibu mwenyekiti wa kamati ya elimu ya chekechea katika kaunti ya Mombasa Suleiman Boma alisema wanapanga kuunda kamati itakayojumuisha wanafunzi ambao watawasilisha malalamishi yao kupitia kamati hiyo.

Aidha, aliongeza kuwa kwa sasa kaunti ya Mombasa haijaamua iwapo itataka kulipwa kwa magari yao yaliyochomwa.

Itakumbukwa kuwa wanafunzi wa TUM walishiriki mgomo majuma matatu yaliyopita na kusababisha uharibifu wa magari mawili ya kuzoa taka ya serikali ya kaunti.