Share news tips with us here at Hivisasa

Mabadiliko ya uteuzi wa mawaziri mbali mbali katika serikali ya Kenya yameleta hisia tofauti miongoni mwa wananchi, huku wengi wakiutaja uteuzi huo kama wa kikabila.

Akizungumza na mwanahabari huyu siku ya Jumatano, mkurugenzi mkuu wa shirika la kijamii la KECOSCE Phyllis Muema alisema mageuzi yaliyofanywa na Rais Uhuru Kenyatta yamefanywa kutokana na misingi ya kikabila wala si kwa misingi ya kitaaluma na uzoefu wa kazi.

Muema alieleza kwamba Rais alifaa kuwapa mawaziri hao kazi kulingana na tajriba zao wala si umarufu walionao.

Katika mabadiliko hayo, Mbunge wa Malindi Dan Kazungu amependekezwa kushikilia wizara ya Madini, huku aliyekuwa Mbunge Mwangi Kiunjuri akipewa wizara ya Ugatuzi ambapo taaluma yake ni Ualimu.

Seneta wa kaunti ya Kericho Charles Keter amepewa wizara ya kawi huku pia taaluma yake ikiwa Ualimu, naye Prof. Jacob Kaimenyi akipewa wizara ya ardhi na taaluma yake ikiwa ni udaktari.

Raisi Uhuru aliwateuwa mawaziri hao siku ya Jumanne, ikiwa hatua inayotajwa kama ya kudhibiti ufisadi nchini.