Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Mwanajeshi mmoja ameambia mahakama kuwa alikatwa kidole wakati wanamgambo wa kundi la Mombasa Republican Council (MRC) walipovamia kambi ya jeshi ya Nyali mwaka wa 2014.

Simon Onyango alisema siku ya Jumanne kuwa vijana zaidi ya 20 walivamia kambi hiyo wakiwa wamejihami kwa mapanga wakiwa na njama ya kuiba bunduki za wanajeshi hao.

Onyango aliongeza kuwa alipata majeraha ya kidole baada ya kushambuliwa na kundi hilo huku bunduki mbili zikikatwa.

Onyango aliyasema haya wakati alipokuwa akitoa ushahidi wake katika mahakama ya Mombasa kwenye kesi inayowakabili vijana walionaswa kuhusika na uvamizi huo.

Uvamizi huo ulitekelezwa mnamo mwaka jana huku mwanajeshi mmoja na wahalifu sita waliuwawa kwenye makabiliano hayo katika kambi hiyo ya jeshi.

Kesi hiyo ingali inaendelea mahakamani huku mashaidi zaidi wakitarajiwa kuitwa kizimbani.