Huneda vijana na akina mama katika eneo bunge la Changamwe, Kaunti ya Mombasa watanufaika katika kujiendeleza kimaisha kupitia mafunzo ya kazi za ujenzi kutoka kwa Halmashauri ya ujenzi nchini, NCA.
Akiongea na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumanne, afisa wa mipango katika afisi ya mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi, aliyemwakilisha katika kongamano hilo la mafunzo, Juma Bakari amesema kwamba mafunzo hayo yanalenga kuwainua kimaisha na kuwakuza kiuchumi wakazi wa eneo hilo.
Kulingana na Bakari, mafunzo hayo yanatarajiwa kuboresha hali ya maisha ya wakazi katika eneo bunge hilo kujipatia miradi mbalimbali itakayowawezesha kupata ajira ikiwemo ujenzi wa barabara na shule.
Bakari amesema kwamba wakazi wa Changamwe wamekumbwa na changamoto nyingi mno kutokana na hali ngumu ya maisha wanayopitia kufutia wengine wao kukosa elimu bora ya kuwawezesha kubuni ajira.
"Tunatarajiwa mafunzo haya ya siku mbili yatawanufaisha kimaisha na kiuchumi wakazi wetu wa eneo bunge la Changamwe kwa kufahamu umuhimu wa kijitafutia ajira mbalimbali," alisema Bakari.
Kwa upande wake Mhandisi Chrispus Dinyo, kutoka halmashauri ya ujenzi nchini, anayetoa mafunzo hayo ni kwamba zoezi hilo la siku mbili litawanufaisha wakazi hao kufuatia vitengo viwili vya mafunzo vinavyotolewa kwa wakazi hao.