Kiongozi wa vijana katika wadi ya Sensi eneo bunge la Kitutu Chache Kaskazini kaunti ya Kisii amewataka vijana kutumia talanta zao kwa kujipatia ajira na kujiendeleza kimaisha.
Akizungumza na mwandishi huyu jumanne mjini Marani, kiongozi wa vijana wadi ya Marani David Omwancha amewaomba vijana wenye talanta kuzitumia na kujiutafutia kazi .
Kiongozi aliwaomba vijana kutokufa moyo wanapogundua talanta zao.
“Naomba kila kijana katika kaunti yetu ya Kisii kutumia talanta kujiendeleza na kutoifanyia mchezo kwani hulipa zaidi," alisema Omwancha.
Wakati huo huo, Omwancha ameiomba serikali ya kaunti kupitia wizara ya utamaduni na michezo kujaribu kila iwezalo kuinua vipaji vya vijana kwani wengi hufa moyo kwa kukosa anayewaunga mkono.
“Naomba kila kijana kujiandikisha na idara ya vipaji ili kuweza kutambulika nchini na kwa kuendeleza talanta,” alisisitiza.
Aidha, Omwancha aliiomba serikali kuanzisha vituo vya kuwafaidi vijana kuendeleza talanta zao kwa kujenga vituo ili kusaidia vijana kuendeleza talanta zao maishani kwani vituo ndio msingi wa kuendeleza talanta.