Vijana kutoka kaunti ya Nyamira wameombwa kutokubali kutumikima na viongozi walioko mamlakani ili kuharibu maisha yao ya siku za mbeleni. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akihutubia makundi ya vijana katika eneo bunge la Kitutu Masaba kule Kemera, muwaniaji wa kiti cha mwakilishi wa kina mama Annet Onsando alishangazwa na idadi ya makundi ya vijana ambayo yamesajiliwa na wizara ya biashara na ushirika kwenye kaunti hiyo, akisema kuwa kusajiliwa kwa idadi kubwa ya vijana kwenye kaunti hiyo ni njia mojawapo ya baadhi ya wanasiasa kuwatumia vibaya vijana kwa manufaa yao wenyewe. 

"Ninaendelea kushangazwa na idadi ya makundi ya vijana yanayoendelea kusajiliwa kwenye kaunti, na kwa maana vijana hao wana misimamo ya kisiasa kuna baadhi ya viongozi wanaopewa pesa kusajili makundi hayo ili kulinda maslahi ya wanasiasa flani," alisema Onsando. 

Mwanasiasa huyo aliongeza kusema kuwa na makundi mengi ya vijana yenye majukumu na maono sawa yanaangamiza ndoto za vijana kujiendeleza na kuafikia malengo fulani katika jamii huku akiongeza kuwahimiza viongozi wa makundi ya vijana kutokubali kutumika na wanasiasa kusajili makundi ya aina hiyo ili kuwafaidi wanasiasa. 

"Mnapokuwa na makundi mengi ya vijana yaliyosajiliwa na yaliyo na majukumu yanayokinzana, hilo hufanya kuwawia vijana vigumu kuafikia malengo fulani maishani na huenda wanasiasa wakawatumia kwa urahisi kuafikia malengo yao huku tukihitaji vijana kuwa katika mstari wa mbele kupigania haki, uwazi na uwajibikaji kutoka kwa viongozi walioko mamlakani," alihimiza Onsando.