Vijana jijini Mombasa wameonywa dhidi ya kujihusisha na ukataji wa nyanya za umeme.
Onyo hilo lilitolewa siku ya Alhamisi, na mshirikishi wa serikali kuu kanda ya Pwani Nelson Marwa, alipokuwa akihutubia wananchi mjini Malindi.
Marwa alisema kuwa kuna vijana wanaokodishwa ili kukata nyaya za umeme mjini Mombasa na kuonya kuwa watakabiliwa vikali na maafisa wa polisi.
Aliongeza kuwa kuna vijana ambao wanatekeleza uhalifu huo ili serikali kuu ionekane imezembea katika kuwahudumia Wakenya.
Marwa alisisitiza kuwa idara ya polisi imepata orodha ya baadhi ya vijana hao na hivi karibuni watasakwa na kufikishwa mahakamani.
Aidha, amewataka Wapwani wote kushirikiana na serikali kuu katika miradi yake ya kimaendeleo ili kukabiliana na umaskini.