Share news tips with us here at Hivisasa

Vijana katika Kaunti ya Mombasa wamehimizwa kujisajili kupata vitambulisho vya kitaifa ili kujisajili kama wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa 2017.

Akizungumza siku ya Jumamosi katika eneo la Changamwe, mwakilishi wadi mteule katika Kaunti ya Mombasa Mary Akinyi, alisema kuwa vijana wengi katika kaunti hiyo hawana vitambulisho, jambo alilosema huwafanya vijana hao kukosa kuwachagua viongozi bora.

Aidha, alisema kuwa ukosefu wa vitambulisho umesababisha vijana kukosa nafasi za ajira.

Akinyi ameitaka idara ya usajali wa watu na vitambulisho kuhakikisha kuwa vijana wote wanapata vitambulisho kabla ya uchaguzi mkuu ujao.