Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vijana wa eneo bunge la Changamwe wametakiwa kuepuka utumizi wa dawa za kulevya na unywaji wa pombe ili kujiepusha na majanga ya uhalifu na kushiriki ngono bila kinga.

Akitoa kauli hiyo, mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi, aliyekuwa akizungumza siku ya Alhamisi alisema mihadharati inawaharibu vijana wengi ambao mwishowe wanajihusisha na vitendo vichafu kama ujambazi na kushiriki ngono bila kinga hivyo basi kuambukizwa ugonjwa Ukimwi.

Aidha, aliongeza kuwa dawa za kulevya zimechangia pakubwa katika kuongezeka visa vya ubakaji katika eneo hilo, jambo alilolitaja kama la kusikitisha na kupotosha adhi ya eneo bunge hilo.

Vilevile, aliwataka vijana kujihusisha na miradi ya kimaendeleo ili kupunguza utumizi wa dawa za kulevya.

Kauli yake inajiri baada ya ripoti kuonesha kuwa kaunti ya Mombasa ina idadi zaidi ya watu 58,000 wanaoishi na virusi vya ukimwi, huku eneo bunge lake likiwa miongoni mwa vijana waoishi na virusi hivyo.