Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Vijana wengi kutoka Kibera wamekuwa wakiacha shule ili kujiunga na biashara ya bodaboda.

Tabia hii imeonekana kuongezeka ambapo vijana wadogo walio na umri wa kadri wamejiunga na biashara hii.

Akiongea katika kijiji cha Sarang’ombe, Kibera, mkazi Johnson Marwa alisema kuwa imefikia kiwango ambacho vijana hawaendi shule ila wanatafuta ajira za kuendesha pikipiki.

“Masomo ni chombo muhimu na ninachukua fursa hii kuwaomba vijana wa Kibera kumaliza masomo kwanza ndio baadaye watafute ajira,’’ alisema Marwa.

Marwa aliwaomba vijana wa eneo hilo kujitahidi katika masomo na kutokubali kupotoshwa na marafiki.