Share news tips with us here at Hivisasa

Vijana wanaofanya kazi na shirika la huduma kwa vijana NYS, eneo la Kongowea wanawalaumu wasimamzi wa mradi huo kwa kuchelewesha malipo yao.

Vijana hao wanalalamikia malipo duni ikilinganishwa na kazi nyingi na ngumu wanazofanya.

Hamisi Mwaruwa, mmoja wa vijana hao alisema jambo hilo linawavunja moyo wa kufanya kazi na kumtaka raisi Kenyatta kuingilia kati ili kutatua tatizo hilo.

Hata hivyo msimamizi wa mradi huo aliyekuwa katika eneo hilo alikanusha madai hayo.