Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vijana katika eneo la Pwani wamehimizwa kujitenga na maswala ya itikadi kali yanayochangia ugaidi na badala yake kuchukua mwelekeo wa kuboresha maisha yao ili kusaidia katika kuliimarisha eneo la Pwani.

Akiwahutubia vijana na wakazi waliyokongamana katika mkutono wa hamasa mjini Mombasa siku ya Jumatatu, Seneta wa Kaunti ya Mombasa Hassan Omar amesema kwamba hali ya vijana wasomi kujiunga na makundi ya kigaidi imechangia hofu kwa wakaazi ya kiusalama na kuna haja ya swala hilo kudhibitiwa.

Kulingana na Omar, ni lazima vijana wenyewe wawe wabunifu wa kikazi kupitia taaluma za masomo walizo nazo, na kujitegemea badala ya kutegemea kuajiriwa, na akafichua kwamba taifa hili limekabiliwa na changamoto za kiuchumi hivyo basi ajira kwa vijana imekuwa nadra.

“Kuna haja ya vijana kujitenga na maswala ya itikadi kali na ugaidi na kuimarisha uchumi wa eneo la pwani badala ya kushawishi vijana na wafuasi wa magaidi na kuliweka eneo hili katika hali ya taharuki,” alisema Sarai.

Wakati uo huo, amewataka vijana hao kuhakikisha kwamba wanawakagua viongozi wa eneo la Pwani na kuwaweka mamlakani wale wanaoyaangazia kwa kina maswala msingi ya kaunti za Pwani yakiwemo elimu, uchumi, na haki msingi za kijamii zikiwemo umiliki wa ardhi.

Kiongozi huyo amewashinikiza wakazi wa eneo la Pwani kuungana na kudumisha amani ili kuona kwamba taifa hili linasonga mbele kimaendeleo na kuboresha uchumi.