Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Vijana katika ukanda wa Pwani wameshauri kujiepusha na baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaowachochea kuzua vurugu na kuharibu usalama wa eneo hili.

Katibu mtendaji katika Baraza la Maimamu na Wahubiri nchini Sheikh Mohamed Khalifa amesema kuwa hatua ambayo baadhi ya viongozi wanatumia kuwalaghai vijana kuzua rapsha kamwe haitasaidia kutatua shida zinazowakumba wakenya bali ni njama ya kujibinafsisha wenyewe.

Akiongea mjini Mombasa siku ya Alhamisi, Sheikh Khalifa amesema kuwa njia mwafaka ya kusuluhisha matitazo yanayowakumba wakenya ni kupitia majadiliano na serikali ili kuona kwamba masuala muhimu yanasuluhishwa kwa amani.

"Tunawaomba vijana kujadiliana na serikali kutatuliwa matatizo yao na kuepukana na viongozi wachochezi kwani huenda wakawalaghai na kuzua vurugu," alisema Sheikh Khalifa.

Kauli ya kiongozi huyo wa kidini imejiri huku eneo la Pwani likikumbwa na mshukosuko kuwa huenda kundi la MRC likazua vurugu na kutatiza usalama wa eneo hili baada ya baadhi ya wafuasi wa kundi hilo kutiwa nguvuni.