Vijana katika eneo bunge la Kisauni wamehimizwa kujitenga na viongozi wabinafsi wasiojali maslahi ya vijana na badala yake kujihusisha na viongozi wenye nia ya kuleta maendeleo masinani.
Akizungumza katika eneo bunge la Kisauni majini Mombasa siku ya Ijumaa, mgombea wa kiti cha eneo bunge hilo katika li uchaguzi wa mwaka ujao, Ali Mbogo alisema kuwa ni jukumu la kila kijana kufikiria maswala muhimu ya kujenga eneo hilo katika siku za usoni.
Mbogo alisema kuwa vijana ndio wenye kulijenga eneo hili na taifa zima kwa jumla ili kuleta maendelea nchini na hususan mashinani na akasema kuwa maswala hayo huletwa na viongozi waadilifu wanaochaguliwa na vijana kwa minajili ya kuleta demokrasia nchini.
“Vijana tafadhali kuweni makini na viongozi wasiopenda kuleta maendeleo mashinani kwa sababu ya kutaka kujibinafsisha wenyewe iwapo mtakuwa maangalifu basi eneo hili litasonga mbele kimaendeleo ndio maana nawasihi muwachague viongozi wachapa kazi.”,alisema Mbogo.
Mbogo alitangaza kuwania kiti cha eneo bunge la Kisauni katika ucgaguzi mkuu ujao wa mwaka m
Hata hivyo viongozi mbali mbali wamejitokeza kuwania kiti hicho ikiwemo mbunge wa eneo hili Rashid Bedzimba, Ali Mbogo, Baya Ruwa na viongozi wengine.
Maelezo ya picha:
Mgombea wa kiti cha eneo bunge hilo katika li uchaguzi wa mwaka ujao, Ali Mbogo alisema kuwa ni jukumu la kila kijana kufikiria maswala muhimu ya kujenga eneo hilo katika siku za usoni.