Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Vijana kutoka mitaa mbali mbali ya Kaunti ya Mombasa wametaja kucheleweshwa kwa hati za vitambulisho ndio sababu kuu ya kuwakwaza katika harakati za kujiandikisha katika kupata kadi za kupigia kura.

Vijana hao ambao wameongea na mwandishi huyu siku ya Jumatatu wametaka utaratibu pamoja na vikwazo vingi vinavyohusiana na kujisajili kupunguzwa ili kuwapa nafasi mwafaka kujiandikisha kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Makundi hayo ya vijana kutoka mitaa ya Tudor, Majengo Ganjoni na Tononoka ambao wengi wao wana asili ya kisomalia walisema kuwa sharti idara au wizara nzima ya usajili wa watu kuliangalia swala hili kwa jicho la ndani na kutoa baadhi ya masharti ambayo walisema inakuwa vigumu kwa baadhi yao ambao wamekulia katika.

Salim Fatiya, mmoja wa vijana hao ambaye alisema kwa muda mrefu amekuwa akifuatilia kupata vitambulisho, lakini hajafanikiwa kwa sababu ya kukosa mojawapo ya hati za mmoja wa mzazi.

“Mimi kila mara nikienda naambiwa nilete hati za vitambulisho ambazo sina, na wenzetu ambao wanapata kujiandikisha huwa vigumu kupata vitambulisho hivyo kwa muda ufaao na tunaiomba idara ya usajili ifanye hima kuweka masharti yao yawe nafuu kwetu angalau tupige kura,” alisema Abdi.

Kwa wito mmoja vijana hao walisihi bunge la Kenya kutafuta utaratibu na kutunga sheria ambazo zitawafaa vijana ili kuwa rahisi kwao kupata hati muhimu za taifa.