Vijana katika eneo la Chaani, eneo bunge la Changamwe wametoa changamoto kwa viongozi wa eneo hilo kushughulikia maslahi ya vijana wakiwa bungeni.
Katika mahojiano na mwanahabari huyu siku ya Jumapili, Moses Mandela ambaye ni mchuuzi wa maji ya kunywa alisema vijana wengi wanakosa kazi na wanataka kupata kazi katika mpango wa kazi kwa vijana.
Aidha, aliongeza kuwa vijana wengi utumia dawa za kulevya baada ya kukosa ajira, hivyo basi kujihusisha pakubwa na ugaidi na wizi.
Vile vile, Mandela aliongeza kuwa kazi ya uuzaji maji ni ngumu, lakini kwa sababu ya kukosa kazi hizo kwa vijana analazimika kukazana na kazi hiyo ili kukidi mahitaji ya familia.
Wengi wa vijana katika maeneo mengi eneo hilo hawana ajira, na wamejiuzisha pakubwa na visa vya uhalifu.