Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Masaba Kaunti ya Kisii Elijah Moindi amewashauri vijana katika eneo bunge lake kufika katika ofisi ya ustawi maeneo bunge CDF katika eneo bunge hilo kujaza fomu ili kukabidhiwa pesa za serikali [mikopo]na kufanyia biashara ili kujiendeleza kimaisha.
Ushauri huo umetolewa baada ya kubainika kuwa idadi kubwa ya vijana wa eneo bunge hilo hawaendi kujaza fomu ili kukabidhiwa pesa hizo, jambo ambalo limesababisha umaskini zaidi.
Moindi alisema vijana wale ambao watakabidhiwa pesa hizo ni wale wako katika vikundi, na kuwashauri wale ambao bado hawajajiunga kwa vikundi kufanya hivyo ili kunufaika.
Akizungumza mnamo siku ya Jumatano katika eneo bunge lake, Mondi alisema kikundi kinastahili kuwa na watu kumi ili kupata fursa ya kukabidhiwa mikopo hiyo ya serikali kujinufaisha wao wenyewe.
“Naomba vijana na watu wengine kufika katika ofisi yangu ya CDF ili kuzaja fomu na kukabidhiwa mikopo ili kujiendeleza kimaisha kupitia biashara,” alisema Moindi.
“Wale ambao watazipata hizo pesa ni wale ambao wako katika vikundi na wito wangu ni kuwa wale ambao bado hawajajiunga kwa vikundi naomba mfanye hivyo na tupunguze umaskini kwa kupata mikopo hiyo ili kujiendeleza kibiashara,” aliongeza Moindi.