Vijana wawili wamefikishwa katika mahakama ya Mombasa na kufunguliwa mashtaka ya wizi wa mabavu.
Upande wa mashtaka uliiambia mahakama siku ya Jumatatu kuwa mnamo Disemba30, 2015, Ayub Bakari na Brain Otieno, wakiwa wamejihami kwa mapanga na visu wanadiwa kumvamia na kumuibia Catherine Kangwe Mbindu.
Washtakiwa wanadaiwa kuiba simu yenye thamani ya shilingi 2,500, kibeti chenye thamani ya shilingi 2,500 na pesa taslimu shilingi 1,800 yote ikiwa ni mali ya Mbindu.
Aidha, wanadaiwa kumtishia kumuua mhasiriwa baada ya kutekeleza wizi huo.
Wote walikanusha madai hayo mbele ya hakimu Richard Odenyo.
Kesi yao itasikilizwa Februari 9, 2016.