Viongozi katika serikali ya kaunti ya Nakuru wametakiwa kutangaza mali yao hadharani.
Ni wito ambao ulitolewa na mwenyekiti wa ODM katika eneo bunge la Nakuru Magharibi Shem Osiago akisema hatua hiyo italeta uwazi katika uongozi wa serikali ya kaunti ya Nakuru.
She alisema yuko tayari kutangaza mali yake kwa umma.
Wakati huo huo, aliwataka wakaazi wa kaunti ya Nakuru waweze kulipa ushuru akisema ushuru huo utawasaidia wakaazi wa kaunti ya Nakuru kupata huduma bora kama vile uwepo wa maji safi ya kunywa na ukarabati wa barabara miongoni mwa huduma zingine.