Viongozi wa kaunti ya Nyamira wamesema hawataandaa kikao na gavana wa wa kaunti hiyo John Nyagarama hadi pale atakapoangazia swala la maendeleo kwenye kaunti hiyo.
Viongozi hao walisema ni sharti Nyagarama aelezee jinsi fedha za kaunti hio zinavyotumika.
Viongozi hao wakiongozwa na mbunge wa eneo bunge la Kitutu Masaba Timothy Bosire walisema gavana anafaa kueleza yale amefanya kabla ya kuandaa kikao kuzungumzia maendeleo.
Msimamo wa viongozi hao ulijiri baada ya gavana kusema kuwa viongozi wa eneo hilo wanafaa kuandaa kikao.
“Tumekuwa tukifanya vikao vingi na gavana Nyagarama kwa muda mrefu lakini yale ambayo tulikuwa tunayazungumzia lazima tuhakikishe yamefanywa kabla ya kuandaa kikao kingine naye,” Bosire alisema.
“Tunahitaji Nyagarama aeleze kati ya yale ameyafanya na ni yapi yamesalia kufanywa na jinsi pesa zimetumika kwa maendeleo,” aliongeza Bosire