Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi wa Pwani wametakiwa kutojihusisha na siasa za mapema, na badala yake kuwa katika mstari wa mbele katika kuimarisha uchumi wa eneo la Pwani.

Akizungumza siku ya Jumanne kwenye ufunguzi wa hoteli ya kimtaifa ya English Point Marina eneo bunge la Nyali, waziri wa utalii, Najib Balala alisema kuwa wapwani wamechoka na siasa na badala yake wanataka kuona maendeleo.

Balala aidha amewataka viongozi hao kutafuta suluhu za kufufua uchumi wa Pwani hasa katika sekta ya utalii na kuachana na siasa zisizo na manufaa kwa mwananchi.

Aidha, ameongeza kuwa wizara yake inajizatiti katika kuimarisha utalii ambao ndio nguzo kuu ya uchumi wa eneo la Pwani.

Kauli hii inajiri baada ya kushudiwa joto la kisiasa eneo la Pwani na viunga vyake katika siku za hivi punde, haswa wakati wa ziara ya Rais Uhuru Kenyatta.