Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Baraza la makanisa katika kaunti ya Nakuru limewataka viongozi hapa nchini kuacha kutia siasa maswala la kanisa. 

Wakihutubia wanahabari mjini Nakuru siku ya Jumanne, viongozi kutoka madhehebu mbali mbali ya kaunti hio walisema maswala ya kanisa hayafai kuendeshwa kidikteta kupitia mapendekezo mapya ambayo yametolewa na mwanasheria mkuu kuhusu udhibiti wa makanisa.

Viongozi hao wakiongozwa na Jotham Opicho walisema wanapinga pendekezo la kuwa na orodha ya kila leo kuhusu shughuli za kanisa na idadi ya wanachama wao, wakisema kwamba kazi yao ni ya kuokoa mioyo mingi zaidi iwezekanavyo kila siku kupitia wokovu.

“Kando na hayo, mapendekezo hayo mapya yanampa msajili mamlaka, ikiwemo ya kufanya ziara ya ghafla kwenye makanisa na kufanya ukaguzi,” Opicho alisema.

“Hii ni serikali inajipa leseni ya kuhakikisha kwamba inakiuka haki za katiba inayopea mkenya uhuru wa kuabudu," Joseph Kamau, askofu wa kanisa la Happy Church Ministries.

Askofu wa kanisa la Chrisco Dan Gitau ameitaka serikali kufanya ushauri zaidi akisema: “Tuko tayari kwa mashauriano na serikali baada ya kukutana na wafuasi wetu wakristu.”