Share news tips with us here at Hivisasa

Huku Wakenya wakijiandaa katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2017, viongozi mbalimbali wa kidini katika eneo la Pwani wamehimizwa kuhubiri amani na kuwaunganisha Wakenya kuwa na uiano.

Afisa wa Nyanjani katika Shirika la Kijamii la Kenya Community Support Centre, Mwalimu Rama amesema kuwa viongozi wa dini mbalimbali wana jukumu kubwa la kuwaunganisha Wakenya kudumisha amani ili taifa hili kuepukana na vurugu zinazowatenganisha. 

Akizungumza mjini Mombasa Rama amesema kuwa Shiriki hilo kwa sasa linaandaa mikutano ya hamasa kwa jamii mashinani kuhakikisha kuwa wanafahamu athiri mbalimbali zinazotokana na mizozo ya kisiasa na kujiepusha na siasa za uchuki na mabishano.

Rama amesema kuwa iwapo viongozi wa kidini watajitokeza waziwazi na kushirikiana na mashirika ya kijamii katika kupeyana hamasa kwa jamii basi kwa kiwango kikubwa usalama na amani utazingatiwa na uchaguzi mkuu ujao utafanyika kwa amani.

Mwanaharakati huyo amewahimiza viongozi wa kidini kutumia fursa ya mikutano ya ibada makanisani na misikitini kuwafundisha vijana na jamii kwa jumla umuhimu wa kutangamana kama jamii moja na kutobaguana katika misngi ya kisiasa, kikabila na kidini.