Baadhi ya viongozi wa kanisa la evangelica lutherlan ELCK tawi la Nyamira wamewaomba viongozi wa makanisa nchini kutojihusisha na visa vya ufisadi vinavyokumba makanisa nchini. 

Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Akihutubia wanahabari mjini Nyamira siku ya Jumatatu, askofu wa kanisa hilo tawi la kusini magharibi mwa Kenya Bakari Keya alisema kuwa visa vya madai ya ufisadi vinavyowakumba viongozi wa makanisa vinaharibu jina la makanisa. 

"Ni ombi langu kwa viongozi wa makanisa kuendesha shughuli za makanisa bila kujihusisha na ufisadi kwa maana visa hivyo vinaharibia jina makanisa na kuleta picha mbaya miongoni mwa wakristo," alisema Keya. 

Keya aidha aliongeza kwa kuwahimiza wakristo kuwasaidia watu wasiojiweza katika jamii hasa kwa kufadhili masomo ya watoto wanaotoka katika familia maskini. 

"Nawaomba wakristo kote nchini kujitokeza kuwasaidia watu wasiojiweza katika jamii hasa kwa kufadhili masomo ya watoto wanaotoka katika familia maskini," aliongezea Keya.