Viongozi wa makanisa kutoka eneo la Olposimoru wamepewa changamoto la kusimama wima na kutoa ushauri kwa pande zote zinazohusika katika mzozo unaozidi kushuhudiwa katika jamii mbili kwa siku kadhaa sasa katika mpaka wa kaunti za Narok na Nakuru.
Ni wito wake Bishop Githu Abraham wa shirika la Beyond Peace and Conflict Resolution Council.
Bishop Githu, aliyeongea na vyombo vya habari mjini Nakuru Jumatatu baada ya kuzuru eneo la Olposimoru mnamo wikendi iliyopita alisema kuwa kulingana na jukumu walilotwikwa viongozi wa kanisa, wana uwezo wa kuwaunganisha jamii hizo husika katika vita hivyo.
“Ni jambo la aibu iwapo viongozi wetu watasimama na kushuhudia maafa sawia na madhara zaidi yakifanyika katika eneo la Olposimoru bila kuchukua hatua zozote,” lisema Githu.
Hata hivyo, amewataka viongozi hao kushirikiana na walinda usalama katika harakati za kusitisha mzozo huo na hivyo kuondoa hofu katika eneo hilo na kuimarisha amani kwa wakenya wote.