Wakazi wa eneo la Kivauni, kaunti ndogo ya Mwala Katika kaunti ya Machakos wamewaomba viongozi wa eneo hilo kuwajibika na kuwajengea wanafunzi wa shule ya chekechea ya Yandaini madarasa ya kusomea. 

Share news tips with us here at Hivisasa

Hii ni baada ya watoto hawa kuwa wakisomea chini ya mti, jambo ambalo huwapa wakati mgumu haswa nyakati za jua au mvua kama sasa. 

Akizungumza katika shule hiyo, kiongozi wa vijana eneo hilo Jeremiah Mwangangi alielezea kusikitishwa kwake kwa kupata watoto hao wakisomea chini ya mti. 

Mwangangi aliwaomba viongozi wa eneo hilo kujitokeza na kuwajengea watoto hawa madarasa, kwani wakati wa mvua hulazimika kujificha kwa majirani au kuadhiriwa na jua wakati wa masomo. 

"Inasikitisha sana kuona watoto walio na kiu cha kusoma wakisomea chini ya mti, ambapo nyakati zingine kama mvua na jua huwapa wakati mgumu," alisema Mwangangi. 

"Ningeomba mbunge wa Mwala Bwana Vincent Musau na  mwakilishi wa Kibauni Frederick Ngunzi kujitokeza na kuwajengea watoto hawa madarasa kwani walichaguliwa kutumikia wananchi," aliongezea Mwangangi.