Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Viongozi wa chama cha ODM eneo la Pwani wamepuzilia mbali madai kuwa mgombea wa kiti cha Malindi kupitia chama hicho Baraka Mtengo hana stakabadhi muhimu za kuwania kiti hicho.

Naibu Kinara wa chama hicho Ali Hassan Joho amemtaka Mtengo kupuzilia mbali madai hayo kwani ni uvumi mtupu.

Aidha, viongozi hao wameapa kwenda mahakamani iwapo gazeti lililochapisha taarifa hiyo halitaomba msahama kwani limemchafulia jina mgombea huyo kuwa hana stakabadhi muhimu zinazohitajika.

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jefwa Kingi, hatua hiyo ni njama ya wahasidi wao kuvurugu uchaguzi huo na kuwapa nafasi kunyakua kiti hicho.

“Sisi tunajua wazi kuwa mwanachama wetu ana stakabadhi halali za kuwania kiti hicho cha ubunge wa Malindi na jinsi gazeti moja nchini lilivyoandika ni njama ya kutuharibia chama na tunataka gazeti hilo kuomba msamaha,” alisema Kingi kwenye mkao na wanahabari mjini Mombasa siku ya Jumamosi.

Kingi amehoji kuwa huenda taarifa hizo zilizochapishwa zilipangwa na viongozi wapinzani ili kuvuruga uchaguzi huo na kunyakua kiti hicho kwa njia ya urahisi.

Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho, Mwakilishi wa kike kaunti ya Mombasa Mishi Mboko, Aisha Jumwa wa kaunti ya Kilifi na Gavana Kingi wamekashifu vikali hatua hiyo na kusema kuwa mgombea huyo ana vyeti halali vya kumruhusu kugombea kiti hicho kilichoachwa wazi na Dan Kazungu ambaye aliteuliwa kuwa Waziri wa Madini.