Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Mwenyekiti wa maktaba nchini Samuel Nyangeso ameomba viongozi wote katika eneo la Kisii kuacha siasa na kutumikia wananchi kimaendeleo.

Kulingana na Nyangeso, kazi ya viongozi ni kufanya maendeleo bali si siasa za kila wakati, huku akisema siasa hurudisha maendeleo nyuma, jambo ambalo si la kufurahisha kwa wakazi na wapiga kura.

Akizungumza siku ya Jumapili mjini Kisii, Nyangeso aliomba viongozi wote kushirikiana pamoja kuhakikisha wananchi wamepata maendeleo yale wanahitaji.

Ata hivyo, aliongezea kuwa idadi kubwa ya viongozi hutoa ahadi wakati wa kutafuta kura, ahadi ambazo sasa amewaomba waweze kuzitimiza ili kunufaisha wakazi .

“Siasa bila maendeleo si siasa za kujenga eneo letu la Kisii na katika taifa letu la Kenya, kila kiongozi anastahili kuacha siasa zisizo za kujenga taifa na kufanyia yale wananchi wanahitaji kufanyiwa kwanza,” alisema Nyangeso.

Wakati huo huo, Nyangeso aliomba wakazi wa Kaunti za Kisii na Nyamira kuungana pamoja na kushirikiana na viongozi kuhakikisha kuwa wanatimiziwa ahadi.

“Naomba wakazi wa kaunti kushirikiana na viongozi ili kuleta maendeleo mengi katika kaunti zetu za Kisii na kujenga taifa la Kenya, tushikane mikono ili kuleta maendeleo,” aliongeza Nyangeso