Viongozi wamekashifu mashambulizi yaliofanywa na genge moja mjini Nakuru katika mtaa wa Flamingo.
MCA wa wadi ya Flamingo Moses Gichangi alisema kisa hico ni cha kusikitisha na kuwataka maafisa wa polisi kufanya uchunguzi ili wote waliohusika kuwajibishwa.
Gavana Kinuthia Mbugua vilevile amekashifu kisa hicho na kuwataka vijana kujihusisha na mambo yatakayowanufaisha kimaisha. “Serikali yangu inaweka mikakati ya kuwasaidia vijana kujihusisha na miradi ya maendeleo,” gavana alisema.
Kundi la vijana wanoarifiwa kujihami kwa mapanga walivamia mtaa huo wa flamingo na kuwakatakata vijana wawili huku wasiwasi ukitanda kuhusu mavamizi hayo.
Aidha inadaiwa washukiwa hao ni kundi la Mungiki. Tayari polisi wamewatia washukiwa wawili mbaroni na wanazuilia kwenye kituo cha Bondeni.