Share news tips with us here at Hivisasa

Viongozi wa kike katika kaunti ya Mombasa wamekosolewa vikali kwa kutozingatia maswala ya mhimu ya wanawake kikamilifu.

Mwenyekiti wa maendeleo ya wanawake katika kaunti ya Mombasa Afiya Rama ameeleza kuwa viongozi wa kike walioko bungeni wamefeli kutetea maslahi ya wanawake na kuchangia hali ngumu kwa wanawake.

Akizungumza mjini Mombasa siku ya Jumatano, Afiya alisema kuwa akina mama wengi mashinani wanapitia hali ngumu ya maisha iliyochangiwa na viongozi hao kukosa kuwahusisha wanawake katika kuangazia maswala muhimu ya uongozi na maendeleo.

Amewahimiza kuwahusisha wanawake wenzao kujadili miswaada mhimu watakayowasilisha katika mabunge yao itakayoleta manufaa kwa wanawake mashinani ili kujihusisha moja kwa maja katika maswala ya kimaendeleo.

"Viongozi wanawake tuliowachagua katika bunge la kaunti ya Mombasa wameshindwa kuitisha hoja muhimu zinazowajali wanawake kutokana na kuwa wabinafsi na hali hiyo imechangia uongozi duni na hali nguma ya maisha kwa wanawake mashinani," alisema Afiya. 

Picha: Mwenyekiti wa maendeleo ya wanawake katika kaunti ya Mombasa Afiya Rama. Amesema kuwa viongozi wanawake waliochaguliwa kaunti ya Mombasa sio wawajibikaji.  Maktaba