Mbunge wa Nyaribari Chache Kaunti ya Kisii Richard Tong’i ameombwa viongozi wote katika eneo la Kisii pamoja na washikadau wengine kujiunga pamoja na kuandaa kikao kuzungumzia changamoto chuo kikuu cha Kisii kinapitia kwa sasa ili kupata suluhisho halisi mapema.
Hii ni baada ya tume inayosimamia vyuo vikuu nchini kudai kufunga matawi 10 kati ya matawi 13 ya chuo hicho kikuu cha Kisii kufuatia kutokuwa na hali nzuri na mahitaji yanayostahili kuwa katika vyuo vikuu.
Akizungumza siku ya Alhamisi katika shule ya upili ya Otamba, Kaunti ya Kisii, Tong’i alisema kuna uwezekano kwa viongozi wote na Gusii na washkadau wengine kuandaa kikao ili kuzungumzia changamoto hizo kabla hazijaenea mbali.
“Mimi naomba viongozi na washkadau wote tuwe na kikao ili kuzungumzia chuo chetu cha Kisii kabla tume ya CUE kufanya kile ilitangaza hapo mapema wiki hii,” alisema Tong’i.
“Naomba naibu chansela wa chuo kikuu cha Kisii Profesa John Akama kupanga jinsi tutakutana ili tuzungumze na tupate suluhu na suluhu hiyo itumwe kwa tume ya CUE kabla ya matawi ya chuo chetu kufungwa bora kinga kuliko kutibu,” aliongeza Tong’i.