Wakazi na wenye mashamba katika shamba la Waitiki kaunti ya Likoni wameitaka idara ya masuala ya shamba kuingilia kati na kumaliza kabisa migogoro katika mashamba hayo.
Haya yamejiri wakati ambapo wanunuzi wawili katika eneo la Mwachamago wametofautiana vikali kuhusu nani mmiliki halali wa shamba hilo.
Akiongea na mwandishi huyu, Mzee Ali amedai kuwa kipande hicho ni chake na hata ashajenga nyumba ambayo anatarajia kuweka madirisha na mlango.
Kwa upande wake Sofia anasema kuwa alikinunua kipande hicho kitambo ila alikuwa hajaanza mjengo.
Matatizo kama haya yamekuwa jambo la kawaida na sasa wakazi wanaomba mbinu kubuniwa ya kutathmini wamiliki halali wa mashamba kabla ya kulipia ada ya shilingi 182,000 ya hati miliki.