Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wavuvi katika kaunti ya Likoni na Mombasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya idadi ya wanunuzi wa samaki kuongezeka maradufu.

Kwa mujibu wa Ahmed Kassim ambaye ni kiongozi wa  kundi moja la kusambaza samaki kwa wenye mabanda ya samaki jijini Mombasa, wakazi wa maeneo hayo wamekumbatia ulaji wa samaki ili kukabili tatizo la upungufu wa mboga.

Ahmed ameongeza kuwa japo kuwa bei ya samaki hairidhishi kwa sasa kwa sababu ya uagizaji wa samaki kutoka nchi jirani, wanapata riziki iliyo ya kutosheleza kwani wamepata kuuza kwa wingi.

Kaunti ya Mombasa imekumbwa na uhaba mkubwa wa mboga za majani na nyanya wakati  huu wa likizo ya Disemba na kupelekea bei ya bidhaa hizo kupanda maradufu.