Wanachama wa mpango wa nyumba kumi katika eneo la Gilgil wanamtaka inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinet kuwazawadi maafisa wa polisi katika eneo hilo ambao wamefanikisha sana kuimarika kwa usalama.
Mwenyekiti wa kundi hilo James Kariuki alisema kuwa uhalifu katika sehemu hiyo umepungua sana hivyo wanapaswa kutambuliwa.
Kulingana naye, maafisa hao wa usalama wamekuwa wakijibu simu zao kwa upesi hivyo kuwafanya wahalifu kushindwa kufanikisha uovu wao.
Kwingineko, kundi moja la kutetea haki za binadamu kutoka Nakuru limemtaka mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma Keriako Tobiko kuharakisha uchunguzi wa mauaji ya jamaa mmoja na afisa mmoja wa AP wiki iliyopita.
Shirika hilo kwa jina Nahurinet limesema uchunguzi wa mauaji ya Emmanuel Bukachi kwa kupigwa risasi unapaswa kupewa uzito zaidi ili familia yake ipate haki.
Hata hivyo shirika hilo limewataka wenyeji wa mtaa wa Lake view pamoja na familia ya marehemu kuwa watulivu uchunguzi unapoendelea.