Share news tips with us here at Hivisasa

Wafanyabiashara wadogo wadogo pamoja na wachuuzi katika eneo la kupima uzani wa malori katika eneo la Gilgil wameirai serikali ya kaunti ya Nakuru kuboresha miundo msingi katika eneo hilo.

Wafanyabiashara hao ambao walizungumza na mwandishi wetu wamesema jumanne hii wamesema kwamba njia ya kupitisha maji taka, pamoja na barabara zilizo jaa mashimo ni baadhi tu ya changamoto zinazowakumba wafanyi biashara hao.

Aidha wamesema kuwa mashimo hayo yamesababishwa na malori ya kubeba mizigo, na wakaelezea hofu yao ya kuingia katika baadhi ya mashimo hayo ambayo hua ni hatari kwa usalama.

Wameongeza ya kwamba maji hayo huwa ni mazingira bora ya mbu ambao husababisha ugonjwa wa malaria, hali ambayo ni tishio kwa afya wa wakaazi na wafanya biashara hao.

Wametoa wito kwa serikali ya kaunti ya nakuru kutafuta suluhu ya haraka ya tatizo hilo.

Itakumbukwa kuwa eneo la Gilgil hususan la kupima uzani wa malori lina uwezo mkubwa kuchangia katika uchumi wa eneo hilo pamoja na kaunti nzima kwa ujumla.