Baadhi ya wafanyabiashara katika jiji la Mombasa wamelalamikia ukosefu wa kontena za kuweka taka, hali ambayo imesababisha kutupwa ovyo hali ambayo imesambaza utapakaji wa uchafu kila mahali kwenye jiji hilo.
Wakiongea siku la Jumanne katika eneo la Ganjoni kupitia kwa mmoja wao, wafanyabiashara hao wakiongezwa na Timothy Kioko walisema kuwa serikali ya kaunti imelipa suala hilo sikio la kufa, akisema kuwa wakazi wa mitaa mbalimbali kutoka kaunti hiyo wamewasilisha lalama zao mara nyingi kupitia kwenye mabaraza ya mji ambao mara nyingi uhudhuriwa na baadhi ya maafisa wa idara.
Mfanyabishara huyo aliongeza kusema kuwa hata mara moja wamewahi kufahamisha mwakilishi wa wa wadi ya Ganjoni kupitia kwenye jumuia ya wakazi na wafanyabiashara wa jiji hilo na wakaahidiwa kuwa kutapatikana suluhu la ukosefu wa kontena hizo.
“Si mara moja tumeweka mkao na wakuu kutoka kwenye kaunti na kuwaambiwa kuongeza kontena kwa sababu baadhi ya wakazi pamoja na wageni wanapokula peremende au chakula chochote kile hutaka kuwa na mahali pa kutupa yale mabaki lakini sasa unapata moja hapa na nyingine baada ya kilimita mbili,” alisema Kioko.
Kulingana na wakazi hao wanapendekeza kuwewepo kwa vifaa hivyo vya kubwaga taka angalau kwa kila maskani na mizunguko ya barabara ili kuwaepusha baadhi ya walaji vyakula kutupa taka sehemu za umma hali ambao wanasema isipochukuliwa maanani huenda ikachafua jiji hilo la kitalii na kuwatia kinyezi wageni wa kitalii na hata kutokomea kwingineko kwa sababu hiyo hiyo.