Gavana wa Kaunti ya Kisii James Ongwae amepongezwa kwa kukamilisha ujenzi wa soko la eneo la Nyakongo lililoko eneo bunge la Kitutu Chache kaskani.
Ujenzi huo wa soko hilo umechukua miaka miwili kukarabatiwa, ambalo limekamilika huku likiwa tayari kufunguliwa na kuzinduliwa rasmi.
Wakizungumza na mwandishi huyu wa habari siku ya Jumatatu katika soko hilo, baadhi ya wafanyibiashara wa soko hilo walimpongeza Ongwae kwa juhudi za kuhakiisha kuwa ujenzi huo umekamilika kwa wakati ufaaao ili kuanza kufanya kazi.
“Tunashukuru gavana wetu kwa kutujengea soko ingawa ujenzi huo umechukua miaka miwili sasa tuko tayari kuanza kufanya biashara kwa kutonyeshewa tena kama hapo awali,” alisema Irene Mose, mfanyibiashara.
Soko hilo ndilokubwa zaidi katika eneo bunge la Kitutu Chache kaskazini, huku mengi yakitarajiwa ili kufaidi wafanyibiashara wa soko hilo.
Wakati uo huo, wafanyibiashara hao waliomba Ongwae pia kuhakikisha vyoo vya soko hilo vimekamilika ili wakati litakapofunguliwa liwe liko na vyoo vya kutoa usaidizi kwa wafanyibiashara.
“Kila kitu kimekamilika lakini tunaona vyoo ndio bado havijashughulikiwa kikamilifu. Tunaomba gavana aweze kuharakisha vimekarabatiwa ili kila kitu kiwe kimekamilika na tuendelee na biashara zetu mbele,” alisema Mogaka Atandi, mfanyibiashara wa ng’ombe.