Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wafanyibiashara kutoka North-Rift wanataka serikali kutengea idara ya usalama fedha zaidi.

Wafayibiashara hao walisema ongezeko la visa vya kudorora kwa usalama nchini ni tishio kwa wawekezaji haswa Kaskazni mwa nchi.

Wakihutubu mjini Eldoret walisema huenda uchumi wa nchi ukasambaratika zaidi iwapo hatua madhubutu hazitachukuliwa mapema ili kukabiliana na changamoto ya usalama nchini.

Mfanyibiashara Joseph Wainaina alipendekeza kupunguzwa kwa fedha ambazo hutengewa ujenzi wa barabara ili sehemu ya fedha hizo ielekezwe kwa maswala ya usalama.

“Iwapo tutaendelea kujenga barabara za kisasa kote nchini bila kuzingatia usalama huenda barabara hizo zikakosa umuhimu kutokana na ongezeko la tishio la usalama,itakuwa vyema zaidi iwapo raisi Uhuru Kenyatta atapunguza fedha ambazo hutengewa barabara ili aslimia fulani ya fedha hizo itumike kuboresha husama katika maeneno ambapo kuna visa vya kudorora kwa usalama,” alisema Wainaina.

Mfanyibishara huyo alipendekeza udhamini zaidi kwa mradi wa nyumba kumi kwa kuajiri watu zaidi mashinani kusimamia mradi huo.

Nao wazee wa mitaani katika kaunti ya Uasin-Gishu walipendekeza serikali kuanza kuwapa marupurupu ili waweze kujikimu kifedha na kushiriki vilivyo katika maswala ya kudumisha usalama.

Wito sawia na huo ulitolewa na mbunge wa Hamisi Charles Gimose ambaye alitaka kubuniwa kwa hazina ya kuwapa marupurupu wazee wa mitaa kote nchini.