Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wafanyibiashara wawili maarufu katika Kaunti nya Nakuru wamearifiwa kutoweka katika hali ya kutatanisha.

Inaarifiwa kuwa wawili hao, Joseph Ngugi Chege almaarufu Jose na Simon Wachira almaarufu Shem walitoweka mwendo wa saa tano asubuhi Ijumaa ya tarehe 22 Januari, baada ya kudaiwa kuchukuliwa na jamaa wanaodaiwa kuwa maafisa wa polisi waliokuwa wamejihami katika mtaa wa White House viungani mwa mji wa Nakuru.

Kulingana na ripoti, Ngugi Chege anafanya kazi katika duka la kuuza nafaka katika soko la Nakuru, huku Wachira akimiliki duka kadhaa mjini Nakuru.

Kufikia sasa, maafisa wa polisi wamepata gari ambalo linadaiwa kuwabeba wawili hao katika kituo cha kibiashara cha Kikopey mjini Gilgil kwenye Kaunti ya Nakuru.

Jamaa na marafiki wa wawili hao sasa wameelezea hofu yao kuwa kutokana na kuwa hawajapata mawasiliano kutoka kwa wawili hao, huku jamaa wa wawili hao wakiarifu wanahabari kwamba baada ya kuripoti tukio hilo kwa polisi wa Gilgil, waliarifiwa kuwa simu za rununu za wawili hao zilikuwa zimezimwa.

Wameongeza kuwa kufikia sasa, hakuna jamaa yeyote ya wawili hao ambaye amepigiwa simu au rafiki yeyote yule ya kutisha fedha ili wawaili hao waachiliwe au ya kuwajuza jambo lolote kuhusiana na wawaili hao.

Kupitia kwa mahojiano kwa njia ya simu na Mbunge wa Nakuru Mashariki David Gikaria, ambaye ni mbunge wa eneo bunge ambako wawili hao wanatoka, amearifu kuwa tukio hilo la wawili hao kutoweka bado halijafahamika vizuri.

Juhudi za wanahabari za kumfikia OCPD wa Nakuru Musa Kongoli kuhusiana na swala hilo hazikufua dafu kwani hakujibu simu yake.