Do you have a lead on a newsworthy story? Share news tips with us here at Hivisasa!

Hatima ya wafanyibiashara wapatao 80 jengo la biashara la Zion Mall mjini Eldoret inayumbayumba baada ya utawala wa kaunti hiyo kuwafurusha.

Utawala huo uliisema uliamua kufurushwa wanabiashara hao kutokana na sababu za kiusalama.

Waziri wa biashara Uasin Gishu Philip Melly alisema licha ya wafanyibiashara husika kupewa leseni za kuendesha biashara katika vyumba hivyo utawala wa kaunti hiyo uliamua kutupilia mbali leseni hizo.

Melly alisema idara ya kutoa leseni ilitoa leseni hizo kabla ya agizo la kutaka wanabiashara husika kuhama.

Kwa mujibu wa Melly ni kwamba hatua hiyo ilichukuliwa baada ya wanabiashara hao kupewa ilani ya kuhama zaidi ya miezi nane iliopita.

“Si kupenda kwetu tufurushe wafanyibiashara hawa kile tunafanya ni kutekeleza sheria ya kuona kwamba vyumba vya chini kwa chini havitumiki kwa biashara badala yake eneo hilo lapaswa kutumiwa kama mahala pa kuegesha magari” alisema

Mapema mwaka jana gavana wa kaunti ya Uasin-Gishu bw Jackson Mandago alitoa iilani ya kuhamisha wanabiashara ambao huendelezea biashara yao katika vyumba vya chini kwa chini.

Licha ya agizo hilo idara ya kutoa leseni iliendelea na kutoa leseni kwa wanabiashara husika.

Bw Melly alisema wanabiashara hao wataruhusiwa kutumia leseni hizo kwingineko mjini humo baada ya kuhamishwa kutoka katika vyumba hivyo.

Nao wanabiashara husika walikosoa utawala wa kaunti kwa kuwapa leseni kuendesha biashara katika eneo hilo ili hali walijua eneo hilo si salama kwa mujibu wa sheria za uhandisi.

Wanabiiashara husika wametishia kufika mahakama kupinga hatua ya kuhamishwa kwao.