Is there a story unfolding in your community? Let Hivisasa know

Wafanyibishara mjini Molo wana matumainim kuwa kuibuka kwa taasisi za elimu kwenye mji huo zitainua hali ya biashara.

Wakiongozwa na mwenyekiti wao Charles Marioko, walisema kuwa miji mingi humu nchini imekuwa kwa kasi kutokana na taasisi za elimu ambazo huwavutia wanafunzi kutoka sehemu mbali mbali.

“Tuna furaha na hatua ya viongozi wa hapa kuinua sekta ya elimu. Sisi kama wafanyibiashara tunajua kuwa taasisi hizi zitakuwa Baraka kwetu,” James Gakuyi alisema

Wakizungumza siku ya Jumamosi baada ya mbunge wa eneo hilo pamoja na chansela wa chuo kikuu cha Kenyatta kufanya kikao, wafanyibiashara hao walikaribisha hatua ya chuo cha Kenyatta kutaka kuanzisha chuo mjini humu.

“Tuna chuo cha KMTC hapa, sasa Kenyatta wakitupa chuo tena sasa tutakuwa na biashara mzuri,” Veronicah Wanja alisema.

Mwenyekiti wa wafanyibiashara mjini humo Charles Marioko alisema mbunge Macharia anafaa kupewa heko kwa juhudi zake.

“Viongozi hawa wamefanya vizuri kufunguo vyuo vya masomo ya juu,wakazi watanufaika pakubwa,” alisema Marioko.