Wafanyikazi saba katika bunge la Kaunti ya Nyamira waliosimamishwa kazi kwa madai ya ufisadi wa Sh30m za NHIF za wawakilishi wa bunge hilo walifikishwa mahakamani siku ya Jumanne.
Miongoni mwa wafanyikazi waliofika mahakamni ni afisa wa pesa za bunge la kaunti Nehemia Nyakundi, katibu wa bunge Zilifanos Nyamora, msimamizi wa bodi ya kuajiri wafanyikazi Enock Nyakundi, naibu katibu Peninah kerama, afisa wa mawasiliano Robert Nyasato, Erick Ong’uti na Duke Onyari.
Wafanyikazi hao walikanusha madai hayo mbele ya Jaji Esther Nyuta.
Jaji Nyuta aliagiza kesi hiyo kusikizwa tena Februari 24, 2016.